13 Watu hao hukata njia yanguhuchochea balaa yangu,na hapana mtu wa kuwazuia.
14 Wanakuja kama kwenye ufa mkubwa,na baada ya shambulio wanasonga mbele.
15 Hofu kuu imenishika;hadhi yangu imetoweka kama kwa upepo,na ufanisi wangu umepita kama wingu.
16 “Sasa sina nguvu yoyote nafsini mwangu;siku za mateso zimenikumba.
17 Usiku mifupa yangu yote huuma,maumivu yanayonitafuna hayapoi.
18 Mungu amenikaba kwa mavazi yangu,amenibana kama ukosi wa shati langu.
19 Amenibwaga matopeni;nimekuwa kama majivu na mavumbi.