20 Nakulilia, lakini hunijibu,nasimama kuomba lakini hunisikilizi.
21 Umegeuka kuwa mkatili kwangu,wanitesa kwa mkono wako wenye nguvu.
22 Wanitupa katika upepo na kunipeperusha;wanisukasuka huku na huko katika dhoruba kali.
23 Naam! Najua utanipeleka tu kifoni,mahali watakapokutana wote waishio.
24 “Je, mtu akikumbwa na maangamizi hainui mkono?Je, mtu akiwa taabuni haombi msaada
25 Je, sikuwalilia wale waliokuwa na taabu?Je, sikuona uchungu kwa ajili ya maskini?
26 Lakini nilipotazamia mema, mabaya yalinipata,nilipongojea mwanga, giza lilikuja.