9 “Na sasa wamenitungia wimbo wa kunizomea,nimekuwa kitu cha dhihaka kwao.
10 Wananichukia na kuniepa;wakiniona tu wanatema mate.
11 Kwa kuwa Mungu amenidhoofisha na kuniaibisha,wamekuwa huru kunitendea wapendavyo.
12 Genge la watu lainuka kunishtakilikitafuta kuniangusha kwa kunitegea.Linanishambulia ili niangamie.
13 Watu hao hukata njia yanguhuchochea balaa yangu,na hapana mtu wa kuwazuia.
14 Wanakuja kama kwenye ufa mkubwa,na baada ya shambulio wanasonga mbele.
15 Hofu kuu imenishika;hadhi yangu imetoweka kama kwa upepo,na ufanisi wangu umepita kama wingu.