1 “Nimejifunga rasmi mimi mwenyewe,macho yangu yasimtazame msichana kwa tamaa.
2 Au je, nangojea nini kutoka kwa Mungu aliye juu?Mungu Mwenye Nguvu ameniwekea kitu gani?
3 Je, maafa hayawapati watu waovuna maangamizi wale watendao mabaya?
4 Je, Mungu haoni njia zangu,na kujua hatua zangu zote?
5 “Kama nimeishi kwa kufuata uongo,kama nimekuwa mbioni kudanganya watu,
6 Mungu na anipime katika mizani ya haki,naye ataona kwamba sina hatia.
7 Kama hatua zangu zimepotoka,moyo wangu ukafuata tamaa za macho yangu;kama mikono yangu imechafuliwa na dhambi,