12 Kosa langu lingekuwa kama moto,wa kuniteketeza na kuangamiza,na kuchoma kabisa mapato yangu yote.
13 Kama nimekataa kesi ya mtumishi wanguwa kiume au wa kike,waliponiletea malalamiko yao,
14 nitafanya nini basi Mungu atakaponikabili?Je, akinichunguza nitamjibu nini?
15 Maana Mungu ndiye aliyeniumba mimi na mtumishi wangu;yeye ndiye aliyetuumba sisi wote.
16 “Je, nimepata kumnyima maskini mahitaji yakeau kuwafanya wajane watumaini bure?
17 Je, nimekula chakula changu peke yangu,bila kuwaachia yatima nao wapate chochote?
18 La! Tangu ujana wangu nimekuwa mlezi wao,tangu utoto wangu nimewaongoza wajane.