19 Je, nilimwona mtu anakufa kwa kukosa nguo,au maskini ambaye hana nguo ya kuvaa,
20 bila kumpa joto kwa mavazi ya manyoya ya kondoo wangunaye akanitakia baraka za shukrani ya moyo?
21 Kama nimenyosha mkono mahakamani dhidi ya yatima,nikijua nitapendelewa na mahakimu,
22 basi, bega langu na lingoke,mkono wangu na ukwanyuke kiwikoni mwake.
23 Maana maafa kutoka kwa Mungu ni kitisho kwangu;mimi siwezi kuukabili ukuu wake.
24 “Je, tumaini langu nimeliweka katika dhahabu,au, nimeiambia dhahabu safi, ‘Wewe ni usalama wangu?’
25 Je, nimepata kufurahia wingi wa utajiri wanguau kujivunia mapato ya mikono yangu?