27 na moyo wangu ukashawishika kuviabudu,nami nikaibusu mikono yangu kwa heshima yake,
28 huo pia ungekuwa uovu wa kuadhibiwa na mahakimumaana ningekuwa mwongo mbele ya Mungu aliye juu.
29 “Je, nimefurahia kuangamia kwa adui yangu,au kufurahi alipopatwa na maafa?
30 La! Sikuruhusu kinywa changu kumtakia mabaya,kwa kumlaani ili afe.
31 Watumishi wangu wote wanasema wazikila mgeni amekaribishwa nyumbani mwangu.
32 Msafiri hakulala nje ya nyumba yangu,nilimfungulia mlango mpita njia.
33 Je nimeficha makosa yangu kama wengine?Je nimekataa kukiri dhambi zangu?