4 Je, Mungu haoni njia zangu,na kujua hatua zangu zote?
5 “Kama nimeishi kwa kufuata uongo,kama nimekuwa mbioni kudanganya watu,
6 Mungu na anipime katika mizani ya haki,naye ataona kwamba sina hatia.
7 Kama hatua zangu zimepotoka,moyo wangu ukafuata tamaa za macho yangu;kama mikono yangu imechafuliwa na dhambi,
8 jasho langu na liliwe na mtu mwingine,mazao yangu shambani na yangolewe.
9 “Kama moyo wangu umevutwa kwa mke wa mtu,kama nimenyemelea mlangoni kwa jirani yangu,
10 basi, mke wangu na ampikie mume mwingine,na wanaume wengine wamtumie.