7 Kama hatua zangu zimepotoka,moyo wangu ukafuata tamaa za macho yangu;kama mikono yangu imechafuliwa na dhambi,
8 jasho langu na liliwe na mtu mwingine,mazao yangu shambani na yangolewe.
9 “Kama moyo wangu umevutwa kwa mke wa mtu,kama nimenyemelea mlangoni kwa jirani yangu,
10 basi, mke wangu na ampikie mume mwingine,na wanaume wengine wamtumie.
11 Jambo hilo ni kosa kuu la jinai,uovu ambao hakimu lazima atoe adhabu.
12 Kosa langu lingekuwa kama moto,wa kuniteketeza na kuangamiza,na kuchoma kabisa mapato yangu yote.
13 Kama nimekataa kesi ya mtumishi wanguwa kiume au wa kike,waliponiletea malalamiko yao,