1 Hapo Mwenyezi-Mungu alimjibu Yobu kutoka dhoruba:
2 “Nani wewe unayevuruga mashauri yangukwa maneno yasiyo na akili?
3 Jikaze kama mwanamume,nami nitakuuliza nawe utanijibu.
4 “Ulikuwa wapi nilipoiweka misingi ya dunia?Niambie, kama una maarifa.
5 Ni nani aliyeweka vipimo vyake, wajua bila shaka!Au nani aliyelaza kamba juu yake kuipima?
6 Je, nguzo za dunia zimesimikwa juu ya nini,au nani aliyeliweka jiwe lake la msingi,