17 Je, umewahi kuoneshwa malango ya kifo,au kuyaona malango ya makazi ya giza nene?
18 Je, wajua ukubwa wa dunia?Niambie kama unajua haya yote.
19 “Je, makao ya mwanga yako wapi?Nyumbani kwa giza ni wapi,
20 ili upate kulipeleka kwenye makao yake,na kuifahamu njia ya kwenda huko kwake.
21 Wewe unapaswa kujua,wewe ambaye umekwisha ishi miaka mingi!
22 “Je, umewahi kuingia katika bohari za theluji,au kuona bohari za mvua ya mawe
23 ambavyo nimevihifadhi kwa ajili ya wakati wa fujo,kwa ajili ya siku ya mapigano na vita?