26 ikasababisha mvua kunyesha nchini kusikoishi mtuna jangwani ambako hakuna mtu,
27 ili kuiburudisha nchi kavu na kamena kuifanya iote nyasi?
28 “Je, mvua ina baba?Au nani ameyazaa matone ya umande?
29 Je, barafu ilitoka tumboni kwa nani?Nani aliyeizaa theluji?
30 Maji hugeuka kuwa magumu kama jiwe,na uso wa bahari ukaganda.
31 “Angalia makundi ya nyota:Je, unaweza kuifunga minyororo Kilimia,au kuvilegeza vifungo vya Orioni?
32 Je, waweza kuziongoza nyota katika majira yake,au kumwongoza Dubu pamoja na watoto wake?