30 Maji hugeuka kuwa magumu kama jiwe,na uso wa bahari ukaganda.
31 “Angalia makundi ya nyota:Je, unaweza kuifunga minyororo Kilimia,au kuvilegeza vifungo vya Orioni?
32 Je, waweza kuziongoza nyota katika majira yake,au kumwongoza Dubu pamoja na watoto wake?
33 Je, wazijua kanuni zinazotawala mbingu;Je, waweza kuzipangia taratibu zao duniani?
34 “Je, waweza kupaza sauti na kuyaamuru mawinguyakufunike kwa mtiririko wa mvua?
35 Je, wewe ukiamuru umeme umulike,utakujia na kusema: ‘Nipo hapa?’
36 Ni nani aliyemjulisha kwarara kujaa kwa mto Niliau aliyemwambia jogoo kwamba mvua inakuja?