4 “Ulikuwa wapi nilipoiweka misingi ya dunia?Niambie, kama una maarifa.
5 Ni nani aliyeweka vipimo vyake, wajua bila shaka!Au nani aliyelaza kamba juu yake kuipima?
6 Je, nguzo za dunia zimesimikwa juu ya nini,au nani aliyeliweka jiwe lake la msingi,
7 nyota za asubuhi zilipokuwa zikiimba pamoja,na wana wa Mungu wakapaza sauti za shangwe?
8 Ni nani aliyeyafunga mafuriko ya bahariwakati yalipozuka na kuvuma kutoka vilindini?
9 Mimi ndiye niliyeifunika bahari kwa mawinguna kuiviringishia giza nene.
10 Niliiwekea bahari mipaka,nikaizuia kwa makomeo na milango,