7 nyota za asubuhi zilipokuwa zikiimba pamoja,na wana wa Mungu wakapaza sauti za shangwe?
8 Ni nani aliyeyafunga mafuriko ya bahariwakati yalipozuka na kuvuma kutoka vilindini?
9 Mimi ndiye niliyeifunika bahari kwa mawinguna kuiviringishia giza nene.
10 Niliiwekea bahari mipaka,nikaizuia kwa makomeo na milango,
11 nikaiambia: ‘Mwisho wako ni hapa, si zaidi!Mawimbi yako ya nguvu yatakomea hapa!’
12 “Yobu, tangu uzaliwe umewahi kuamuru kupambazuke?na kulifanya pambazuko lijue mahali pake,
13 ili lipate kuikamata dunia kwa pembe zakena kuwatimulia mbali waovu waliomo?