1 “Je, wajua mbuzi wa milimani huzaa lini,au umewahi kuona kulungu akizaa?
2 Je, wajua huchukua mimba kwa muda gani,au siku yenyewe ya kuzaa waijua?
3 “Wajua wakati watakapochuchumaa kuzaa,wakati wa kuzaa watoto wao?
4 Watoto wao hupata nguvu,hukua hukohuko porini,kisha huwaacha mama zao na kwenda zao.