17 kwa sababu nilimfanya asahau hekima yake,wala sikumpa sehemu yoyote ya akili.
18 Lakini akianza kukimbia,humcheka hata farasi na mpandafarasi.
19 “Je, Yobu, ndiwe uliyewapa farasi nguvu,ukawavika shingoni manyoya marefu?
20 Je, ni wewe unayemfanya farasi aruke kama nzige?Mlio wake wa maringo ni wa ajabu!
21 Huparapara ardhi mabondeni kwa pupa;hukimbilia kwenye mapigano kwa nguvu zake zote.
22 Farasi huicheka hofu, na hatishiki;wala upanga hauwezi kumrudisha nyuma.
23 Silaha wachukuazo wapandafarasi,hugongana kwa sauti na kungaa juani.