26 “Je, mwewe amejifunza kwako jinsi ya kuruka,na kunyosha mabawa yake kuelekea kusini?
27 Je, tai hupaa juu kwa amri yako,na kuweka kiota chake juu milimani?
28 Tai hufanya makazi yake juu ya miamba mirefu,na ncha kali za majabali ndizo ngome zake.
29 Kutoka huko huotea mawindo,macho yake huyaona kutoka mbali.
30 Makinda yake hufyonza damu;pale ulipo mzoga ndipo alipo tai.”