4 Watoto wao hupata nguvu,hukua hukohuko porini,kisha huwaacha mama zao na kwenda zao.
5 “Nani aliyemwacha huru pundamwitu?Nani aliyewaacha waende kwa kuwafungua?
6 Mimi niliwapa jangwa liwe makao yao,mbuga zenye chumvi kuwa makazi yao.
7 Hujitenga kabisa na makelele ya miji,hasikilizi kelele ya kumfanyisha kazi.
8 Hutembeatembea milimani kupata malisho,na kutafuta chochote kilicho kibichi.
9 “Je, nyati atakubali kukutumikia?Au je, atakubali kulala zizini mwako?
10 Je, waweza kumfunga nyati kamba kulima shamba,au avute jembe la kulimia?