8 Hutembeatembea milimani kupata malisho,na kutafuta chochote kilicho kibichi.
9 “Je, nyati atakubali kukutumikia?Au je, atakubali kulala zizini mwako?
10 Je, waweza kumfunga nyati kamba kulima shamba,au avute jembe la kulimia?
11 Je, utamtegemea kwa kuwa ana nguvu nyingina kumwacha akufanyie kazi zako nzito?
12 Je, wamtazamia nyati akuvunie mavuno yako,na kuleta nafaka mahali pa kupuria?
13 “Mbuni hupigapiga mabawa yake kwa madaha,lakini hawezi kuruka kama korongo.
14 Mbuni huyaacha mayai yake juu ya ardhiili yapate joto mchangani;