1 Mwenyezi-Mungu akaendelea kumwambia Yobu:
2 “Je, wewe mwenye kuchunguza makosa utashindana na Mungu Mwenye Nguvu?Wewe unayebishana nami Mungu, basi jibu mambo hayo!”
3 Kisha Yobu akamjibu Mwenyezi-Mungu:
4 “Mimi sifai kitu nitakujibu nini?Naufunga mdomo wangu.
5 Nilithubutu kusema na sitasema tena.Nilisisitiza lakini sitaendelea kusema zaidi.”
6 Hapo Mwenyezi-Mungu akamjibu kutoka kimbunga:
7 “Jikaze kama mwanamume.Nitakuuliza, nawe utanijibu.