10 “Basi, jioneshe kuwa na fahari na ukuu,ujipambe kwa utukufu na fahari.
11 Wamwagie watu hasira yako kuu;mwangalie kila mwenye kiburi na kumwangusha.
12 Mwangalie kila mwenye kiburi na kumporomosha,uwakanyage waovu mahali walipo.
13 Wazike wote pamoja ardhini;mfunge kila mmoja kwa kifungo cha kifo.
14 Hapo nitakutambua,kwamba nguvu yako mwenyewe imekupa ushindi.
15 “Liangalie lile dude Behemothi,nililoliumba kama nilivyokuumba wewe.Hilo hula nyasi kama ng'ombe,
16 lakini mwilini lina nguvu ajabu,na misuli ya tumbo lake ni imara.