18 Mifupa yake ni mabomba ya shaba,viungo vyake ni kama pao za chuma.
19 “Hilo ni la kwanza la ajabu kati ya viumbe vyangu!Ni mimi Muumba wake niwezaye kulishinda.
20 Milima wanamocheza wanyama wote wa porinihutoa chakula chake.
21 Hujilaza chini ya vichaka vya miiba,na kujificha kati ya matete mabwawani.
22 Hujisitiri katika vivuli vya vichaka vya miibana vya miti iotayo kando ya vijito.
23 Mto ukifurika haliogopi,halitishiki hata mto Yordani ukilifurikia kinywani.
24 Nani awezaye kuliziba macho na kuliteka?Nani awezaye kulitoboa pua kwa mtego?