22 Hujisitiri katika vivuli vya vichaka vya miibana vya miti iotayo kando ya vijito.
23 Mto ukifurika haliogopi,halitishiki hata mto Yordani ukilifurikia kinywani.
24 Nani awezaye kuliziba macho na kuliteka?Nani awezaye kulitoboa pua kwa mtego?
25 Je, waweza kuvua dude Lewiyathani kwa ndoana,au kuufunga ulimi wake kwa kamba?
26 Je, unaweza kulitia kamba puani mwake,au kulitoboa taya kwa kulabu?
27 Je, wadhani litakusihi uliachilie?Je, litazungumza nawe kwa upole?
28 Je, litafanya mapatano nawe,ulichukue kuwa mtumishi wako milele?