25 Je, waweza kuvua dude Lewiyathani kwa ndoana,au kuufunga ulimi wake kwa kamba?
26 Je, unaweza kulitia kamba puani mwake,au kulitoboa taya kwa kulabu?
27 Je, wadhani litakusihi uliachilie?Je, litazungumza nawe kwa upole?
28 Je, litafanya mapatano nawe,ulichukue kuwa mtumishi wako milele?
29 Je, utacheza nalo kama ndege,au kulifunga kamba licheze na wajakazi wako?
30 Wadhani wavuvi watashindania bei yake?Je, wafanyabiashara watathubutu kulikata na kugawana?
31 Je, waweza kuichoma ngozi yake kwa mikuki,au kichwa chake kwa mfumo wa kuvua samaki?