4 “Mimi sifai kitu nitakujibu nini?Naufunga mdomo wangu.
5 Nilithubutu kusema na sitasema tena.Nilisisitiza lakini sitaendelea kusema zaidi.”
6 Hapo Mwenyezi-Mungu akamjibu kutoka kimbunga:
7 “Jikaze kama mwanamume.Nitakuuliza, nawe utanijibu.
8 Je, unataka kweli kubatilisha hukumu yangu,kuniona nina hatia ili wewe usiwe na hatia?
9 Je, una nguvu kama mimi Mungu?Waweza kunguruma kwa sauti kama yangu?
10 “Basi, jioneshe kuwa na fahari na ukuu,ujipambe kwa utukufu na fahari.