12 Puani mwake hufuka moshi,kama vile chungu kinachochemka;kama vile magugu yawakayo.
13 Pumzi yake huwasha makaa;mwali wa moto hutoka kinywani mwake.
14 Shingo yake ina nguvu ajabu,litokeapo watu hukumbwa na hofu.
15 Misuli yake imeshikamana pamoja,imara kama chuma wala haitikisiki.
16 Moyo wake ni mgumu kama jiwe,mgumu kama jiwe la kusagia.
17 Linapoinuka, mashujaa hushikwa na woga,kwa pigo moja huwa wamezirai.
18 Hakuna upanga uwezao kulijeruhi,wala mkuki, mshale au fumo.