19 Kwake chuma ni laini kama unyasi,na shaba kama mti uliooza.
20 Mshale hauwezi kulifanya likimbie;akitupiwa mawe ya teo huyaona kama makapi.
21 Kwake, rungu ni kama kipande cha bua,hucheka likitupiwa fumo kwa wingi.
22 Tumbo lake ni kama limefunikwa na vigae vikali;hukwaruza na kurarua udongo kama chombo cha kupuria.
23 Bahari huisukasuka kama maji yachemkayo,huifanya itoe povu kama chupa ya mafuta.
24 Lipitapo huacha nyuma alama inayongaa;povu jeupe huonekana limeelea baharini.
25 Duniani hakuna kinachofanana nalo;hilo ni kiumbe kisicho na hofu.