21 Kwake, rungu ni kama kipande cha bua,hucheka likitupiwa fumo kwa wingi.
22 Tumbo lake ni kama limefunikwa na vigae vikali;hukwaruza na kurarua udongo kama chombo cha kupuria.
23 Bahari huisukasuka kama maji yachemkayo,huifanya itoe povu kama chupa ya mafuta.
24 Lipitapo huacha nyuma alama inayongaa;povu jeupe huonekana limeelea baharini.
25 Duniani hakuna kinachofanana nalo;hilo ni kiumbe kisicho na hofu.
26 Huwaona kuwa si kitu wote wenye kiburi;hilo ni mfalme wa wanyama wote wakali.”