7 Mgongo wake umefanywa kwa safu za ngaozilizoshikamana pamoja kama kwa mhuri,
8 Kila moja imeshikamana na nyingine,hata hewa haiwezi kupenya katikati yake.
9 Yameunganishwa pamoja,hata haiwezekani kuyatenganisha.
10 Likipiga chafya, mwanga huchomoza,macho yake humetameta kama jua lichomozapo.
11 Kinywani mwake hutoka mienge iwakayo,cheche za moto huruka nje.
12 Puani mwake hufuka moshi,kama vile chungu kinachochemka;kama vile magugu yawakayo.
13 Pumzi yake huwasha makaa;mwali wa moto hutoka kinywani mwake.