1 Kisha Yobu akamjibu Mwenyezi-Mungu:
2 “Najua kwamba waweza kila kitu,lolote unalokusudia haliwezi kuzuiliwa.
3 Ulisema kuwa nilithubutu kutatiza mpango wako kijinga.Kweli nilitamka kitu ambacho sikuelewamambo ya ajabu mno kwanguambayo sikuwa ninayajua.
4 Uliniambia nisikilize nawe utaniambia;kwamba utaniuliza nami nikujibu.