1 “Binadamu anayo magumu duniani,na siku zake ni kama siku za kibarua!
2 Yeye ni kama mtumwa atamaniye kivuli,kama mwajiriwa angojaye kwa hamu mshahara wake.
3 Basi nimepangiwa miezi na miezi ya ubatili,yangu ni majonzi usiku hata usiku.
4 Nilalapo nasema, ‘Nitaamka lini?’Kwani saa za usiku huwa ndefu sana;nagaagaa kitandani mpaka kuche!