1 “Binadamu anayo magumu duniani,na siku zake ni kama siku za kibarua!
2 Yeye ni kama mtumwa atamaniye kivuli,kama mwajiriwa angojaye kwa hamu mshahara wake.
3 Basi nimepangiwa miezi na miezi ya ubatili,yangu ni majonzi usiku hata usiku.
4 Nilalapo nasema, ‘Nitaamka lini?’Kwani saa za usiku huwa ndefu sana;nagaagaa kitandani mpaka kuche!
5 Mwili wangu umejaa mabuu na uchafu;ngozi yangu imekauka na kutokwa na usaha wa jipu.
6 Siku zangu zapita kasi kuliko gurudumu la mshonaji,nazo zafikia mwisho wake bila matumaini.
7 “Kumbuka, maisha yangu ni pumzi tu;jicho langu halitaona jema lolote tena.