10 Anayeondoka harudi tena kwa jamaa yake,na pale alipokuwa anaishi husahaulika mara.
11 “Kwa hiyo sitakizuia kinywa changu kuongea;nitasema kwa msongo wa roho yangu,nitalalamika kwa uchungu wa nafsi yangu.
12 Je, mimi ni bahari au dude la baharinihata uniwekee mlinzi?
13 Nikisema, ‘Kitanda kitanipumzisha,malazi yangu yatanipunguzia malalamiko yangu,’
14 wewe waja kunitia hofu kwa ndoto,wanitisha kwa kuniletea maono;
15 hata naona afadhali kujinyonga,naona heri kufa kuliko kupata mateso haya.
16 Nayachukia maisha yangu;sitaishi milele.Niacheni, maana siku zangu ni pumzi tu!