12 Je, mimi ni bahari au dude la baharinihata uniwekee mlinzi?
13 Nikisema, ‘Kitanda kitanipumzisha,malazi yangu yatanipunguzia malalamiko yangu,’
14 wewe waja kunitia hofu kwa ndoto,wanitisha kwa kuniletea maono;
15 hata naona afadhali kujinyonga,naona heri kufa kuliko kupata mateso haya.
16 Nayachukia maisha yangu;sitaishi milele.Niacheni, maana siku zangu ni pumzi tu!
17 Binadamu ni nini hata umjali?Kwa nini hata unajishughulisha naye?
18 Wewe waja kumchunguza kila asubuhi,kila wakati wafika kumjaribu!