13 Nikisema, ‘Kitanda kitanipumzisha,malazi yangu yatanipunguzia malalamiko yangu,’
14 wewe waja kunitia hofu kwa ndoto,wanitisha kwa kuniletea maono;
15 hata naona afadhali kujinyonga,naona heri kufa kuliko kupata mateso haya.
16 Nayachukia maisha yangu;sitaishi milele.Niacheni, maana siku zangu ni pumzi tu!
17 Binadamu ni nini hata umjali?Kwa nini hata unajishughulisha naye?
18 Wewe waja kumchunguza kila asubuhi,kila wakati wafika kumjaribu!
19 Utaendelea kuniangalia hata lini,bila kuniacha hata nimeze mate?