7 “Kumbuka, maisha yangu ni pumzi tu;jicho langu halitaona jema lolote tena.
8 Anayeniona sasa, hataniona tena,punde tu ukinitazama nitakuwa nimetoweka.
9 Kama wingu lififiavyo na kutowekandivyo nao watu washukavyo kuzimu bila kurudi.
10 Anayeondoka harudi tena kwa jamaa yake,na pale alipokuwa anaishi husahaulika mara.
11 “Kwa hiyo sitakizuia kinywa changu kuongea;nitasema kwa msongo wa roho yangu,nitalalamika kwa uchungu wa nafsi yangu.
12 Je, mimi ni bahari au dude la baharinihata uniwekee mlinzi?
13 Nikisema, ‘Kitanda kitanipumzisha,malazi yangu yatanipunguzia malalamiko yangu,’