13 “Wapo wengine waovu wasiopenda mwanga,wasiozifahamu njia za mwanga,na hawapendi kuzishika njia zake.
14 Mwuaji huamka mapema alfajiri,ili kwenda kuwaua maskini na fukara,na usiku ukifika, kazi yake ni kuiba.
15 Mzinifu naye hungojea giza liingie;akisema, ‘Hakuna atakayeniona;’kisha huuficha uso wake kwa nguo.
16 Usiku wezi huvunja nyumba,lakini mchana hujifungia ndani;wala hawajui kabisa mwanga ni nini.
17 Kwao wote giza nene ni mwanga wa asubuhi;wao ni marafiki wa vitisho vya giza nene.
18 “Lakini mwasema:‘Waovu huchukuliwa haraka na mafuriko ya maji,makao yao hubaki kuwa nchi iliyolaaniwa;hakuna aendaye kwenye mashamba yao ya mizabibu.’
19 Kama theluji inavyoyeyuka katika joto na ukamendivyo Kuzimu kunavyowanyakua waovu.