1 Hatimaye Yobu aliamua kuongea, akailaani siku aliyozaliwa.
2 Yobu akasema:
3 “Ilaaniwe siku ile niliyozaliwa;usiku ule iliposemwa, ‘Mwana amechukuliwa mimba’
4 Siku hiyo na iwe giza!Mungu juu asijishughulishe nayo!Wala nuru yoyote isiiangaze!
5 Mauzauza na giza nene yaikumbe,mawingu mazito yaifunike.Giza la mchana liitishe!
6 Usiku huo giza nene liukumbe!Usihesabiwe katika siku za mwaka,wala usitiwe katika idadi ya siku za mwezi.
7 Naam, usiku huo uwe tasa,sauti ya furaha isiingie humo.