10 Maana usiku huo haukulifunga tumbo la mama,wala kuficha taabu nisizione.
11 Mbona sikufa nilipozaliwa,nikatoka tumboni na kutoweka?
12 Kwa nini mama yangu alinizaa?Kwa nini nikapata kunyonya?
13 Maana ningekuwa nimezikwa, kimya;ningekuwa nimelazwa na kupumzika,
14 pamoja na wafalme na watawala wa dunia,waliojijengea upya magofu yao;
15 ningekuwa pamoja na wakuu waliokuwa na dhahabu,waliojaza nyumba zao fedha tele.
16 Au, mbona sikuwa kama mimba iliyoharibika,naam, kama mtoto aliyezaliwa mfu?