4 Siku hiyo na iwe giza!Mungu juu asijishughulishe nayo!Wala nuru yoyote isiiangaze!
5 Mauzauza na giza nene yaikumbe,mawingu mazito yaifunike.Giza la mchana liitishe!
6 Usiku huo giza nene liukumbe!Usihesabiwe katika siku za mwaka,wala usitiwe katika idadi ya siku za mwezi.
7 Naam, usiku huo uwe tasa,sauti ya furaha isiingie humo.
8 Walozi wa siku waulaani,watu stadi wa kuligutua dude Lewiyathani waulaani!
9 Nyota zake za pambazuko zififie,utamani kupata mwanga, lakini usipate,wala usione nuru ya pambazuko.
10 Maana usiku huo haukulifunga tumbo la mama,wala kuficha taabu nisizione.