33 Je nimeficha makosa yangu kama wengine?Je nimekataa kukiri dhambi zangu?
34 Sijaogopa kusimama mbele ya umati wa watu,wala kukaa kimya au kujifungia ndani,eti kwa kuogopa kutishwa na dharau zao.
35 Laiti angekuwapo mtu wa kunisikiliza!Naweza kutia sahihi yangu katika kila nilichosema.Namwambia Mungu Mwenye Nguvu anijibu!Laiti mashtaka wanayonitolea maadui zangu yangeandikwa!
36 Ningeyavaa kwa maringo mabeganina kujivisha kichwani kama taji.
37 Ningemhesabia Mungu kila kitu nilichofanya,ningemwendea kama mwana wa mfalme.
38 Kama nimeiiba ardhi ninayoilima,nikasababisha mifereji yake iomboleze,
39 kwa kufaidika na mazao yake bila kulipana kusababisha kifo cha wenyewe,