36 Ningeyavaa kwa maringo mabeganina kujivisha kichwani kama taji.
37 Ningemhesabia Mungu kila kitu nilichofanya,ningemwendea kama mwana wa mfalme.
38 Kama nimeiiba ardhi ninayoilima,nikasababisha mifereji yake iomboleze,
39 kwa kufaidika na mazao yake bila kulipana kusababisha kifo cha wenyewe,
40 basi miiba na iote humo badala ya ngano,na magugu badala ya shayiri.”Mwisho wa hoja za Yobu.