15 “Je, shoka litajigamba dhidi ya anayelitumia?Msumeno waweza kujivuna dhidi ya mwenye kukata nao?Ni kana kwamba fimbo ingeweza kumwinua anayeishika,au mkongojo kumwinua mwenye kuutumia!”
16 Kwa hiyo, Bwana Mwenyezi-Mungu wa majeshi,atawaletea askari wao ugonjwa wa kuwakondesha,na fahari yao itateketezwa kama kwa moto.
17 Mungu aliye mwanga wa Israeli atakuwa kama moto,Mtakatifu wa Israeli atakuwa mwali wa motoambao kwa siku moja utateketeza kila kitu:Miiba yake na mbigili zake pamoja.
18 Misitu yake ya fahari na mashamba yake mazuri,Mwenyezi-Mungu atayaangamiza yote;itakuwa kama mtu aliyemalizwa na ugonjwa.
19 Miti itakayobaki msituni mwake itakuwa michache sanahata mtoto mdogo ataweza kuihesabu.
20 Siku ile wazawa wa Yakobo watakaobaki, naam, Waisraeli watakaosalia hawatalitegemea tena taifa lililowaadhibu, bali watamtegemea kabisa Mwenyezi-Mungu, Mtakatifu wa Israeli.
21 Wazawa wa Yakobo wachache watakaobaki watamrudia Mungu Mkuu.