1 Maono aliyoyaona Isaya, mwana wa Amozi, kuhusu Yuda na mji wa Yerusalemu, nyakati za utawala wa Uzia, Yothamu, Ahazi na Hezekia, wafalme wa Yuda.
2 Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Sikilizeni enyi mbingu,tega sikio ee dunia.Mimi nimewalea wanangu wakakua,lakini sasa wameniasi!
3 Ngombe humfahamu mwenyewe,punda hujua kibanda cha bwana wake;lakini Waisraeli hawajui,watu wangu, hawaelewi!”
4 Ole wako wewe taifa lenye dhambi,watu waliolemewa na uovu,wazawa wa wenye kutenda maovu,watu waishio kwa udanganyifu!Nyinyi mmemwacha Mwenyezi-Mungu,mmemdharau Mtakatifu wa Israeli,mmefarakana naye na kurudi nyuma.
5 Kwa nini huachi uasi wako?Mbona wataka kuadhibiwa bado?Kichwa chote ni majeraha matupu,na moyo wote unaugua!
6 Toka wayo hadi kichwa hamna penye nafuu,umejaa majeraha na vidonda vitoavyo damu,navyo havikuoshwa, kufungwa wala kutiwa mafuta.
7 Nchi yenu imeharibiwa kabisa;miji yenu imeteketezwa kwa moto.Wageni wananyakua nchi yenu mkiona kwa macho,imeharibiwa kama uharibifu wa Sodoma.
8 Mji Siyoni umeachwa kama kibanda shambani,kama kitalu katika shamba la matango,kama mji uliozingirwa.
9 Mwenyezi-Mungu wa majeshi asingalituachia wachache,tungalikwisha kuwa kama watu wa Sodoma,tungalikuwa hali ileile ya Gomora.
10 Sikilizeni neno la Mwenyezi-Munguenyi watawala waovu kama wa Sodoma!Sikilizeni mafunzo ya Mungu wetuenyi watu waovu kama wa Gomora!
11 Mwenyezi-Mungu asema hivi;“Wingi wa tambiko zenu ni kitu gani kwangu?Nimezichoka sadaka zenu za kondoo wa kuteketezwana mafuta ya wanyama wenu wanono.Sipendezwi na damu ya fahali,wala ya wanakondoo, wala ya beberu.
12 Mnapokuja mbele yangu kuniabudunani aliyewataka mkanyagekanyage nyua zangu?
13 Msiniletee tena matoleo yenu yasiyo na maana;ubani ni chukizo kwangu.Acheni kufanya sikukuu za mwezi mpya,Sabato na mikutano mikubwa ya ibada;sikubali ibada zilizochanganyika na dhambi.
14 Sikukuu zenu za mwezi mpya na nyinginezomoyo wangu wazichukia.Zimekuwa mzigo mzito kwangu,nami nimechoka kuzivumilia.
15 “Mnapoinua mikono yenu kuombanitauficha uso wangu nisiwaone.Hata mkiomba kwa wingi sitawasikia,maana mikono yenu imejaa damu.
16 Jiosheni, jitakaseni;ondoeni uovu wa matendo yenu mbele yangu.Acheni kutenda maovu,
17 jifunzeni kutenda mema.Tendeni haki,ondoeni udhalimu,walindeni yatima,teteeni haki za wajane.”
18 Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Njoni, basi, tuhojiane.Ingawa mna madoa mekundu ya dhambi,mtatakaswa na kuwa weupe kama theluji;madoa yenu yajapokuwa mekundu kama damu,mtakuwa weupe kama sufu.
19 Mkiwa tayari kunitii,mtakula mazao mema ya nchi.
20 Lakini mkikaidi na kuniasi,mtaangamizwa kwa upanga.Mimi, Mwenyezi-Mungu, nimesema.”
21 Jinsi gani mji uliokuwa mwaminifusasa umegeuka kuwa kahaba!Wakati mmoja haki ilitawala humo,lakini sasa umejaa wauaji.
22 Fedha yenu imekuwa takataka;divai yenu imechanganyika na maji.
23 Viongozi wako ni waasi;wanashirikiana na wezi.Kila mmoja anapenda hongo,na kukimbilia zawadi.Hawawatetei yatima,haki za wajane si kitu kwao.
24 Kwa hiyo asema Bwana Mwenyezi-Mungu,Mwenye Nguvu wa Israeli:“Nitawamwagia maadui zangu hasira yangu,nitawalipiza kisasi wapinzani wangu.
25 Nitanyosha mkono wangu dhidi yenu;nitayeyusha uchafu wenu kabisa,na kuondoa takataka yenu yote.
26 Nitawapeni waamuzi wenu kama kwanzana washauri wenu kama pale awali.Ndipo Yerusalemu utakapoitwa ‘Mji wa Uadilifu’utaitwa ‘Mji Mwaminifu’”
27 Mji Siyoni utakombolewa kwa haki,uadilifu utawaokoa watakaotubu humo.
28 Lakini waasi na wenye dhambiwote wataangamizwa pamoja;wanaomwacha Mwenyezi-Mungu watateketezwa.
29 Mtaionea aibu hiyo mialoni mliyoipenda sana;mtafadhaika kwa sababu ya bustani mlizofurahia.
30 Mtakuwa kama mwaloni unaonyauka majani;kama shamba lisilo na maji.
31 Wenye nguvu watakuwa kama majani makavu,matendo yao yatakuwa kama cheche za moto.Watateketea pamoja na matendo yao,wala hapatakuwa na mtu wa kuwaokoa.