1 “Teremka uketi mavumbiniewe Babuloni binti mzuri!Keti chini pasipo kiti cha enziewe binti wa Wakaldayo!Tokea sasa hutaitwa tena mwororo wala nadhifu.
2 Twaa mawe ya kusagia, usage unga kama mtumwa!Vua utaji wako, ukavue na mavazi yako!Pandishia vazi lako miguuni, ukavuke mito.
3 Watu watauona uchi wako;naam, wataiona aibu yako.Mimi nitalipiza kisasi,wala sitamhurumia yeyote.”
4 Mkombozi wetu ndiye Mtakatifu wa Israeli;Mwenyezi-Mungu wa majeshi ndilo jina lake.
5 Mwenyezi-Mungu asema:“Ewe taifa la Wakaldayolililo kama binti mzuri,keti kimya na kutokomea gizani.Maana umepoteza hadhi yakoya kuwa bimkubwa wa falme.
6 Niliwakasirikia watu wangu Israeli,nikawafanya watu wangu kuwa haramu.Niliwatia mikononi mwako,nawe hukuwaonea huruma;na wazee uliwatwisha nira nzito mno.
7 Ulijisemea moyoni: ‘Nitakuwa malkia milele’,nawe hukuyatafakari mambo yanayotokea,wala kufikiri mwisho wake.
8 “Sasa, basi, sikiliza ewe mpenda anasa,wewe unayedhani kuwa u salama,na kujisemea: ‘Ni mimi tu,na hakuna mwingine isipokuwa mimi.Kamwe sitakuwa mjane,wala sitafiwa na wanangu.’
9 Haya yote mawili yatakupata,ghafla, katika siku moja:Kupoteza watoto wako na kuwa mjane,ijapokuwa una wingi wa uchawi wako,na nguvu nyingi za uganga wako.
10 “Ulijiona salama katika uovu wako;ukajisemea, ‘Hakuna mtu anayeniona.’Hekima na elimu yako vilikupotosha,ukajisemea moyoni mwako, ‘Mimi ndiye;hakuna mwingine anayenishinda.’
11 Lakini maafa yatakupataambayo hutaweza kujiepusha nayo.Balaa litakukumbaambalo hutaweza kulipinga;maangamizi yatakujia ghaflaambayo hujapata kamwe kuyaona.
12 Endelea basi na uganga wako,tegemea wingi wa uchawi wako.Wewe uliyapania hayo tangu ujana wakoukitumainia kwamba utafanikiwaau kusababisha kitisho kwa watu!
13 Wewe umejichosha bure na washauri wako.Basi, na wajitokeze hao wanajimu wakuokoe!Wao huzigawa mbingu sehemusehemu,huzichunguza nyotana kubashiri kila mwezi yatakayokupata.
14 “Kumbuka, wao ni kama mabua makavu:Moto utayateketezea mbali!Hawawezi hata kujiokoa wenyewembali na ukali wa moto huo.Moto huo si wa kujipatia joto,huo si moto wa kuota!
15 Ndivyo watakavyokuwa hao uliowategemea hivyo,hao uliojishughulisha nao tangu ujana wako.Watatangatanga kila mmoja njia yake;hakuna hata mmoja atakayeweza kukuokoa.”