1 Kauli ya Mungu dhidi ya jangwa kando ya bahari.Kama vimbunga vinavyovuma kutoka kusini,wavamizi wanakuja kutoka jangwani,kutoka katika nchi ya kutisha.
2 Nimeoneshwa maono ya kutisha,maono ya watu wa hila watendao hila,maono ya watu waangamizi wafanyao maangamizi.Pandeni juu vitani enyi Waelamu;shambulieni enyi Wamedi!Mungu atakomesha mateso yoteyaliyoletwa na Babuloni.
3 Kwa maono hayo nimeingiwa na hofu kubwa,uchungu mwingi umenikumba;kama uchungu wa mama anayejifungua.Maumivu yamenizidi hata siwezi kusikia;nimefadhaika hata siwezi kuona.
4 Moyo unanidunda na woga umenikumba.Nilitamani jioni ifikelakini ilipofika ikawa ya kutetemesha.
5 Chakula kimetayarishwa,shuka zimetandikwa,sasa watu wanakula na kunywa.Ghafla, sauti inasikika:“Inukeni enyi watawala!Wekeni silaha tayari!”
6 Maana Bwana aliniambia,“Nenda ukaweke mlinzi;mwambie atangaze atakachoona.
7 Akiona kikosi, wapandafarasi wawiliwawili,wapandangamia na wapandapunda,na awe macho;naam, akae macho!”
8 Kisha huyo mlinzi akapaza sauti:“Bwana, nimesimama juu ya mnara wa ulinzi mchana kutwa,nimeshika zamu usiku kucha!”
9 Tazama, kikosi kinakuja,wapandafarasi wawiliwawili.Wanasema: “Babuloni umeanguka! Umeanguka!Sanamu zote za miungu yakezimetupwa chini na kuvunjwavunjwa!”
10 Ewe Israeli, watu wangu,enyi mliotwangwa na kupurwa kama nafaka.Sasa nimewaambieni mambo niliyoyasikiakwa Mwenyezi-Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli.
11 Kauli ya Mungu dhidi ya Duma.Ninasikia mtu ananiita kutoka Seiri:“Mlinzi, nini kipya leo usiku?Kuna kipya chochote leo usiku?”
12 Nami mlinzi nikajibu:“Asubuhi inakuja, kadhalika na usiku;ukitaka kuuliza, uliza tu;nenda urudi tena.”
13 Kauli ya Mungu dhidi ya Arabia.Enyi misafara ya Dedani,pigeni kambi leo usiku kwenye nyika za Arabia.
14 Enyi wakazi wa nchi ya Tema,wapeni maji hao wenye kiu;wapelekeeni chakula hao wakimbizi.
15 Maana wamekimbia mapanga,mapanga yaliyochomolewa,pinde zilizovutwa na ukali wa mapigano.
16 Maana Bwana aliniambia hivi: “Katika muda wa mwaka mmoja, bila kuzidi wala kupungua, fahari yote ya Kedari itakwisha.
17 Wapiga upinde wachache kati ya mashujaa wa watu wa Kedari ndio watakaosalia. Mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, nimenena.”