1 Laiti ungalizipasua mbingu ukashuka chini,milima ikakuona na kutetemeka kwa hofu!
2 Ingeteketea kama moto uchomavyo kichaka,kama vile moto uchemshavyo maji.Njoo upate kuwajulisha maadui zako jina lakonayo mataifa yatetemeke kwa kuwako kwako!
3 Wakati ulipotenda maajabu ambayo hatukutazamia,ulishuka chini nayo milima ikatetemeka ilipokuona.
4 Tangu kale hakuna aliyepata kuonawala kusikia kwa masikio yake;hakuna aliyepata kumwona Mungu aliye kama weweatendaye mambo kwa ajili ya wale wanaomtegemea!
5 Wewe waja kuwasaidia watendao haki kwa furaha,wanaokukumbuka na kuzingatia njia zako.Ulitukasirikia tulipokuwa wenye dhambi;sisi tumeasi kwa muda mrefu.
6 Sote tumekuwa kama watu walio najisi;matendo yetu yote mema ni kama nguo chafu.Sote tunanyauka kama majani,uovu wetu watupeperusha kama upepo.
7 Hakuna hata mmoja anayekuja kukuomba;hakuna anayejishughulisha kukutafuta.Wewe unauficha uso wako mbali nasi,umetuacha tukumbwe na maovu yetu.
8 Hata hivyo, ee Mwenyezi-Mungu, wewe ni Baba yetu.Sisi ni kama udongo, wewe ni mfinyanzi.Sisi sote ni kazi ya mikono yako.
9 Usitukasirikie mno, ee Mwenyezi-Mungu,usiukumbuke uovu wetu daima!Ukumbuke kwamba sisi sote ni watu wako!
10 Miji yako mitakatifu imekuwa nyika;Siyoni umekuwa mahame,Yerusalemu umekuwa uharibifu.
11 Nyumba yetu takatifu na nzuri,ambamo wazee wetu walikusifu,imeteketezwa kwa moto.Mahali petu pote pazuri pamekuwa magofu.
12 Je, kwa hayo yote utajizuia usifanye kitu?Je, utaendelea kunyamaza tu, ee Mwenyezi-Mungu,na kututesa kupita kiasi?