1 “Wewe Beli umeanguka;Nebo umeporomoka.Wakati mmoja watu walibeba sanamu zenu.Sasa wanazibeba mgongoni mwa wanyama,hao wanyama wachovu wamelemewa.
2 Nyinyi mmeanguka na kuvunjika,hamwezi kuviokoa vinyago vyenu;nyinyi wenyewe pia mtapelekwa uhamishoni!
3 “Sikilizeni enyi wazawa wa Yakobo,nisikilizeni enyi mabaki ya watu wangu wa Israeli.Mimi niliwatunzeni tangu mlipozaliwa;niliwabebeni tangu tumboni mwa mama yenu.
4 Mimi ni yuleyule hata katika uzee wenu;hata katika uzee wenu mimi nitawabeba.Nilifanya hivyo kwanza,nitafanya hivyo tena.Nitawabeba nyinyi na kuwaokoa.
5 “Mtanifananisha na nani, tufanane?Je, mwaweza kunilinganisha na nani, tulingane?
6 Watu humimina dhahabu kutoka mifuko yao,hupima fedha kwenye mizani zao,wakamwajiri mfua dhahabu atengeneze sanamukisha huisujudu na kuiabudu!
7 Hujitwisha sanamu hiyo mabegani, wakaibeba,kisha huiweka mahali pake, ikakaa papo hapo;kamwe haiwezi hata kusogea kutoka hapo ilipo.Mtu akiililia, haiwezi kumwitikia,wala haiwezi kumwokoa mtu katika taabu zake.
8 “Kumbukeni jambo hili na kutafakari,liwazeni akilini mwenu enyi wakosefu.
9 Kumbukeni mambo niliyotenda hapo kale!Mimi ndimi Mungu na hakuna mwingine;naam, mimi ni Mungu, wala hakuna mwingine kama mimi.
10 Nilitangaza mambo ya mwisho tangu mwanzo,tangu kale nilitangaza mambo yatakayotukia.Lengo langu litatimia;mimi nitatekeleza nia yangu yote.
11 Ninamwita tai wangu kutoka mashariki,naam, msiri wangu kutoka nchi ya mbali.Mimi nimenena na nitayafanya;mimi nimepanga nami nitatekeleza.
12 “Nisikilizeni, enyi wenye vichwa vigumu,nisikilizeni enyi mlio mbali na ukombozi.
13 Siku ya kuwakomboa naileta karibu,haiko mbali tena;siku ya kuwaokoeni haitachelewa.Nitauokoa mji wa Siyoni,kwa ajili ya Israeli, fahari yangu.