25 Maana bado kitambo, nayo hasira yangu itapita na ghadhabu yangu itawageukia Waashuru.
26 Mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi na nitawachapa kama nilivyowachapa Wamidiani kwenye jabali la Orebu. Nitanyosha fimbo yangu juu ya bahari kuwachapa kama nilivyowafanya Wamisri.
27 Wakati huo, mzigo waliowabebesha nitauondoa na nira waliyowatia shingoni mwenu itavunjwa.”Adui amepanda kutoka Rimoni,
28 amefika mjini Ayathi.Amepitia huko Migroni,mizigo yake ameiacha Mikmashi.
29 Amekwisha pita kivukoni,usiku huu analala Geba.Watu wa Rama wanatetemeka kwa hofu,wakazi wa Gibea, mji wa Shauli, wamekimbia.
30 Pazeni sauti enyi watu wa Galimu!Tegeni sikio enyi watu wa Laisha!Jibuni enyi wenyeji wa Anathothi!
31 Watu wa Madmena wako mbioni,wakazi wa Gebimu wanakimbilia usalama.